MUHTASARI WA KITABU: Andamo ni diwani ya tungo za ushairi zilizoandikwa na Mohammed Ghassani kwa muongo mmoja kuanzia miaka ya mwanzoni ya 1990 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000. Ni tungo zinazoogelea pamoja naye kwenye bahari ya uzoefu wa mwanzo wa ujana kuelezea hadithi yake ya maisha, mtazamo wake juu ya yale yaliyokuwa yakitokea mbele ya macho yake na ufahamu wake kwa ulimwengu. Aliyekuwa Katibu wa Kamati ya Fasihi na Utamaduni ya Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA), Bwana Abbas Mdungi, wakati akikabidhi ripoti ya mswaada wa diwani hii mwezi Oktoba 2003, aliandika hivi: .."..Mshairi ameibuni kazi yake kwa ustadi mkubwa kama kwamba ni mweledi katika utunzi ilhali hii ndiyo kazi yake ya kwanza kabisa. Mitindo aliyotumia ni mingi na mizuri ambayo inatafautiana na wakati wengine kushabihiana....Kwenye lugha, ametumia lugha ya ushairi - nyoofu, nzuri na telezi... Maudhui, bila shaka, ameyatumia vizuri kuweza kuelimisha jamii akijikita kwenye masuala ya utamaduni, siasa na uchumi, ingawa utamaduni umekuwa sura kubwa zaidi.....Kwa kawaida, washairi wa Afrika huzikita dhamira zao katika migogoro ya kimapenzi, kindoa, kidini, kikazi, kinyonyaji, kidemokrasia, uongozi mbaya, umangimeza, njaa, umasikini na maradhi, naye kwa ujumla amefanikiwa sana katika hilo...." Kwa hivyo, ndani ya Andamo, sio tu muna mwangwi wa sauti ya kijana anayejaribu kuiwasilisha hadithi yake kwa hadhira kwa njia ya kishairi, lakini pia ishara ya kuibuka kwa kipaji cha aina yake kwenye uwanja wa fasihi ya Kiswahili.